0
Nuhu Mziwanda ambae ni mchumba wa mwanamuziki na muigizaji Shilole (Shishi baby) ameomba radhi jana kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kupost picha ambayo inaonyesha maungo ya ndani ya mp3nzi wake huyo walipokuwa wakioga.
Picha hiyo ilimuonyesha Shilole akiwa kifua wazi. Kwa mujibu wa Nuhu Mziwanda amesema kuwa alipost picha hiyo ili apate Kiki kwa ajili ya video yake mpya Zimataa ambayo bado haijatoka mpaka sasa.


Baada ya juzi usiku Nuhu Mziwanda kupost picha hiyo kwenye ukurasa wake mtandaoni mashabiki walionyesha kutofurahishwa na kitendo hicho na wengihne kufikia hatua ya kutukana huku wengine wakidai kuwa amemdharirisha mp3nzi wake huyo ambae ni mama wa watoto wawili.



"Naomba niombe radhi kwa waliochukizwa na picha niliopost usiku wa jana.Lakini naweza sema pia ile ilikuwa ni video yangu mpya ya wimbo wangu wa Zimataa.So ilikuwa ni promotion picture.Ila mwisho wa maneno yangu ni kuomba radhi kwa lililotokea."-Mziwanda aliandika.



Nadhani “Promo” wameipata.

Post a Comment

 
Top