0
Rapper Nay wa Mitego, wiki ijayo anatarajia kuachia kazi yake mpya ambapo amesema ni kati ya collabo aliyofanya na Diamond Platnumz au na msanii wa Nigeria.
Nay ameiambia Bongo5 kuwa, bado yupo kwenye upembuzi ili kujua ni kitu gani kitakuja kati ya kazi hizo.

“Kuna uwezekano tukawa tunaachia wimbo mpya wiki ijayo,” amesema. “Ni kitu ambacho watu walikuwa wanakisubiria kwa muda sana na inawezekana ikawa ni wimbo mkubwa sana. Kuna project na Diamond na kuna project ile niliyofanya nje ya nchi moja kazi ya hizo inaweza ikatoka.”

“Kama unavyojua niliingia studio tena na Diamond na kufanya kazi mpya hivi karibuni lakini japo haijaisha ni ngoma kubwa na nina matumani makubwa kuhusu hii kazi. Lakini ninachotaka next week watu wajue kuna kitu kikubwa kinakuja. Tuna release wimbo mpya, kwahiyo ndani ya siku mbili hizi mambo yate yatakuwa wazi baada ya mipango kukaa sawa. Kwahiyo kati ya project hizo mbili moja itatoka.”

Post a Comment

 
Top