0

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi Sabrina Omary ‘Sabby’ wakipozi kimahaba.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Cyrill Kamikaze ‘Cyrill’ na Mbongo Muvi Sabrina Omary ‘Sabby’ hivi karibuni walinaswa katika ufukwe wa Hoteli ya Golden Tulip, Masaki jijini Dar wakiwa kimahaba na hivyo kuzidisha tetesi kuwa wanatoka kimapenzi.Chanzo chetu makini kilisema wawili
hao walionekana hotelini hapo wakiwa eneo la kuogelea na walipomaliza walihamia katika viti ambako sasa walikumbatiana kimahaba kana kwamba hakuna mtu anayewaona.

Kwa nyakati tofauti walipoulizwa kuhusu tetesi za kuwa wapenzi na ushahidi wa picha, kila mmoja alikana, wakidai zitakuwa ni picha za kutengenezwa kwa sababu mchezo huo umekuwa maarufu siku hizi huku Sabby akisisitiza kuwa angefika ofisini ili kujiridhisha na picha hizo ndipo aweze kuzungumza, kitu ambacho hakukifanya.

Post a Comment

 
Top