0

Wiki iliyopita nilikuwekea story kuhusu mastaa wa muziki wa Marekani, Pharell Williams, Robin Thicke na T.I walikuwa na kesi Mahakamani, shitaka lililokuwa linawahusu mastaa hao ni ishu ya kutuhumiwa kukopi wimbo wa marehemu Marvin Gaye, ambapo watoto wa mwanamuziki huyo walifungua kesi hiyo.

Wimbo ambao wanatuhumiwa kuukopi ni wimbo wa ‘Blurred Lines‘, moja ya hits ambazo zimependwa sana duniani pamoja na kushiriki Tuzo kadhaa pamoja na kushinda NAACP Image Awards kama wimbo bora wa collabo mwaka 2014.

Wimbo huo unadaiwa kuwa jamaa walikopi wimbo wa ‘Got to Give It Up‘ ambao ulikuwa hits pia ya Marvin Gaye miaka ya 1970.

Hukumu ambayo imetolewa ni kulipa dola Mil. 7.3, hukumu hiyo inawahusu Robin Thicke na Pharrell Williams ambao kwenye hatimiliki wanatambulika kama waandishi na wamiliki wa wimbo huo.

Post a Comment

 
Top