Muimbaji wa muziki nchini, Ruta Bushoke ambaye muda mwingi alikuwa nchini Afrika Kusini, amesema baba yake, Maxi Bushoke, mwanamuzki wa siku nyingi aliyepitia bendi ya Sikinde ndiye role model wake.
Maxi Bushote ndiye aliyeandika nyimbo kama ‘Mesenja Kaleta Balaa’ na ‘Christina’ akiwa na Sikinde.
Akiongea na kwenye kipindi cha Ubaoni cha Gadner G Habash wa EFM wakati akitambulisha wimbo wake mpya, ‘Nimekumanya’, alisema baba yake ndio mwanamuziki ambaye amekuwa akimuangalia tokea akiwa mdogo na pia ndio anayemkubali zaidi.
“Unajua baba yangu ndio mwanamuziki ambaye namkubali sana na pia amekuwa akinishauri sana, ndio maana hata leo ukiniweka na live band yoyote ile naimba bila wasiwasi. Unajua Baba yangu hadi akukubali ni kazi sana maana mwanzo alikuwa ananiambia bado sijui kuimba lakini sasa hivi ananikubali na kuniamini. Nilifanya kazi sana kumshawishi hadi anikubali. Kuna muda hadi niliona kama dingi hanipendi vile, lakini kumbe alikuwa ananijenga ili niwe mwanamuziki mzuri na sio ilimradi tu msanii,” alisema Bushoke.
Katika hatua nyingine, Bushoke alisema alipokuwa Afrika Kusini, amejifunza vitu vingi kuhusu muziki kwakuwa alikuwa akikutana na watu tofauti tofauti. Pamoja na kuwa na changamoto nyingi, Bushoke anazichukulia kama sehemu ya kumjenga zaidi katika kazi yake ya muziki na pia kumjenga kwa yeye kufanya kazi nzuri zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment