0
Rapper Young Killer Msodoki amesema kuwa ameamua kutokutoa nyimbo mara kwa mara kama ilivyokuwa kipindi yuko na management, kwa lengo la kutowachosha mashabiki wake.
Wimbo wake wa mwisho kuachia kama single rasmi ni ‘Kumi na Tatu’ aliyofanya na Fid Q ambayo ilitoka Octoba 2014.

“Nimejaribu kutengeneza mazingira ya kutosikika mara kwa mara kutokana na kutowachosha mashabiki, lakini hata nikikaa kimya ule ujio unaoweza ukawa unakuja unaweza ukawa wa kishindo” ameiambia Bongo5.

“Naamini ukimya mwingine unaweza ukawa na mafanikio na ukimya mwingine unaweza ukawa hauna mafanikio, lakini ukimya wangu wa sasa hivi na kukaa kimya muda mrefu naamini kunaweza kukawa na mafanikio mbele yangu.” Alisema Young Killer.

“Young Killer hajawahi kukaa mauda mrefu kama hivi hajatoa ngoma, kipindi cha nyuma wakati nipo na management muda kama huu Young Killer alikuwa ameshatoa ngoma mbili tokea alipotoa Kumi na tatu, mi toka mwaka jana mwezi wa kumi sijatoa ngoma mpaka sasa hivi inamaana ni miezi sita, kipindi niko na management nilikiuwa natoa ngoma kila baada ya miezi mitatu. Lakini kwa muda huu nimekaa miezi sita sijatoa ngoma na show kama kawaida napiga kwahiyo naamini najitengeneza uimara zaidi.”

Rapper huyo wa Mwanza amesema anatarajia kuuvunja ukimya huo muda si mrefu kwa kuanza kuachia nyimbo alizokuwa akiziandaa kwa kipindi chote hicho.

“Mwaka huu nadhani ni mwaka ambao unaweza ukawa na mafanikio kutokana na kazi ambazo nitazitoa, ndani ya wiki hii au wiki ijayo nitaanza kuwafyatulia kazi na ni kazi baada ya kazi hadi mwaka uishe”.

Post a Comment

 
Top