0
Kila msanii aliyefanikiwa huwa ana historia inayokuwa na mambo mengi ambayo mashabiki hawayafahamu ambayo aliwahi kuyapitia kabla ya kupata umaarufu. Upande wa hit maker wa ‘Siachani Nawe’ Barakah Da Prince amesema kipindi cha nyuma aliwahi kuonja kidogo muziki wa kurap katika harakati zake za kutoka.
Akizungumza kupitia Planet Bongo ya EATV, Barakah amesema kuwa ana mpango wa kufanya ngoma ya Hip Hop na Roma, na kuongeza kuwa kuna uwezekano wa Fareed Kubanda a.k.a Fid Q kusimama kwenye chorus ya ngoma hiyo.

Alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho Dullah Ambua kama huo ni mpango tu au tayari ameshafanya mazungumzo na Roma kuhusu kazi hiyo, Barakah alisema kuwa tayari wameshazungumza na kukubaliana kufanya project hiyo.

Aliongeza kuwa haimaanishi kuwa anabadili muziki anaoufanya, bali ni kuwaonesha tu mashabiki kile alichowahi kukifanya kipindi cha nyuma.

Kingine ambacho wengi hawakifahamu amesema kuwa yeye na Mo Music waliwahi kuwa kundi moja huko jijini Mwanza kabla kila mmoja wao hajaanza kutafuta njia zake za kutoka.

Post a Comment

 
Top