0
Baada ya Ben Pol kuingia kwenye mkataba mpya wa usimamizi wa kazi zake na kampuni ya Panamusiq hivi karibuni, muimbaji huyo wa R&B ameanza kuweka mikakati ya kuupeleka muziki wake kimataifa.
Ben Pol amesema exclusively kuwa hatua ya kwanza ya safari ya kuupeleka muziki wake kimataifa, anatarajia kufanya collabo na msanii wa kike kutoka Nigeria ambaye hakupenda kumtaja kwa sasa kwa madai kuwa bado ni mapema.

“Bado tuko kwenye mazungumzo ya mwisho na tumeshatumiana nyimbo, ameomba maelekezo, na ameridhia lakini sasa hivi kumtaja kidogo nimeambiwa nisubiri, lakini yeye ameonyesha interest ya kutaka kufanya huo wimbo na ameupenda ameomba atumiwe mashairi atumiwe beat, kwahiyo kuna uwezekano ikawa na mafanikio.” alisema Ben Pol.

Hit maker huyo wa ‘Sofia’ ameongeza kuwa licha ya kuwa anamshirikisha msanii wa Nigeria lakini wimbo huo utakuwa na mahadhi ya R&B kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye nyimbo zake.

Kama mipango ikifanikiwa basi hiyo ndio itakuwa collabo ya kwanza kubwa kwa Ben Pol kufanya na msanii wa kimataifa.

Post a Comment

 
Top