0
Mzuka wa siasa unazidi kuwaingia wasanii wengi wa muziki nchini. Keisha ni mmoja wao.
 Keisha amesema naye pia ana mpango wa kuingia rasmi kwenye kuwania nafasi ya uongozi wa kisiasa japo inaweza isiwe mwaka huu.

“Napenda sana harakati za siasa, nimeshawahi kufikiria lakini bado sikupata jibu sahihi,” amesema. “Kwahiyo sasa hivi siwezi kusema nipo tayari ama vipi. Lakini nikiwa tayari nitaweka wazi kila kitu. Mimi ni mwana-CCM damu kabisa nimekunywa maji ya bendera.”

Miongoni mwa wasanii watakaogombea ubunge mwaka huu ni pamoja na Profesa Jay na Afande Selle.

Post a Comment

 
Top