0
Rapper kutoka Morogoro, Stamina aliye mbioni kuachia album yake ‘Mount Uluguru’ amesema ameamua kuachia album yake ‘Mount Meru’ si kwasababu ya kutegemea impe fedha, bali anataka kutengeneza profile.
Stamina amesema kuwa kupitia album hiyo anahitaji kutengeneza profile ya muziki wake.

“Kuna leo na kesho unapotea kwenye muziki watu watakukumbuka na nini,? amehoji rapper huyo. “Lakini kama una albUm watasikiliza kazi zako. Kwahiyo album ni profile ya msanii, tatizo watu wangi wanaangalia hela, wanaangalia sokoni kutakuwaje? Hakuna habari za sokoni, hata kama usipouza lakini utakuwa umetengeneza profile katika muziki wako.”

“KwaAHiyo wadau wasubiri album ya ‘Mount Uluguru’ itakuwa na nyimbo 23. Nyimbo zangu zilizotoka lazima ziwepo kwenye album ndo maana watu hawajui kwanini nyimbo zangu nilikuwa nazitoa kwa mfululizo vile. Nyimbo yangu iliyonitoa kwenye muziki ilikuwa inaitwa Kabwela, iliyofuata Alisema, ikaja Najuta Kubalehe ukijumilisha unapata ‘Kabwela alisema najuta kubalehe’. Baada ya hapo nikaja na Wazo la Leo, ikaja Kamwambie Mwenzio, baada ya hapo itakuja Mguu pande mguu sawa, ukijumlisha unapata Wazo la leo Kamwambie mwenzio mguu pande mguu sawa.’ Kwahiyo nyimbo zangu zote zipo hivyo, kwahiyo watu wangu watafute hii album.”

Pia Stamina amewataka mashabiki wa muziki wake wa Morogogo kuungana naye katika uzinduzi huo wa album utakaofanyika mkoani Morogoro Jumamosi, May 30 . Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Afande Selle.

Post a Comment

 
Top