0
Staa mkongwe wa filamu za Bongo, Vincent “Ray” Kigosi ametoa sababu ya kuendelea kuwa single licha ya kuwa anaendelea kuongeza idadi ya birthday alizosheherekea toka kuzaliwa kwake.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa katika mahojiano maalum, Ray alisema amekuwa akipangua mawazo ya kuoa kila wakati kutokana na ugumu wa kumpata mwanamke ambaye hatampa stress kama zinazowapata baadhi ya watu.

Alisema, kwa kuwa suala la kuoa ni jambo nyeti, halihitaji kukurupuka na hicho ndicho kimemfanya mpaka leo asiingie kwenye maisha ya ndoa.

“Unajua hili suala la ndoa ni sensitive ‘nyeti’ sana, halihitaji kukurupuka, linakutaka ukiingia kwenye uhusiano umchunguze vizuri huyo uliyempata ili kujiaminisha kwamba, hatakusumbua.

“Hilo ndilo linalonifanya niwe singo mpaka leo, najua wengi wananishangaa lakini kwa kifupi ugumu wa kumpata mweza sahihi ndiyo sababu ya kutooa mpaka leo,” alisema Ray.

Alipoulizwa kwamba, ina maana kwa wapenzi wake waliopita wakiwemo Ruth Suka ‘Mainda’, Blandina Chagula ‘Johari na Hans Chuchu hakuna aliyeona anafaa kuwa mke, msanii huyo alicheka sana kisha akasema: “Wewee, acha mambo yako.”

 

Post a Comment

 
Top