Siku chache baada ya kuachia video/wimbo mpya ‘Nusu Nusu’, rapper kutoka Weusi Joh Makini amesema mpango wa awali ulikuwa kwenda Afrika Kusini kushoot video ya wimbo mpya aliomshirikisha msanii wa Hip Hop kutoka Nigeria, lakini mambo yalibadilika dakika za mwisho kabla ya safari.
Joh Makini amesema kuwa siku mbili kabla ya kusafiri kwenda Afrika Kusini , msanii huyo wa Nigeria alipata safari ya Marekani hivyo kushindwa kwenda kufanya video ya Joh na ndipo ilimbidi Mwamba kuchagua wimbo mwingine wa kufanyia video ambao ni ‘Nusu Nusu’.
“Ilikuwa naenda kufanya wimbo ambao nimefanya na msanii mmoja wa Hip Hop kutoka Nigeria sitamtaja kwa sasa hivi, ila imefika kama siku mbili kabla ya safari ya South jamaa akawa amepata safari ya Marekani. Kwahiyo ikawa ratiba zake zikawa zinam-tight ikawa haiwezekana yeye kuwahi South Africa kwaajili ya video, kwahiyo ilibidi chapchap niangalie kwenye benki yangu ya ngoma ikabidi nichague ngoma nyingine fasta. Lakini huo wimbo tayari ulikuwa umeshatumwa na script ilikua imeshaandikwa tulikua tumeshakubaliana na director jinsi ambavyo video itakuwa kila kitu.” Alisema Joh Makini.
Ngoma ya Joh Makini aliyomshirikisha rapper wa Nigeria inaitwa ‘On My Way’ ambayo imesikika mwanzoni mwa video ya ‘Nusu Nusu’ wakati Joh anampigia simu Nareel.
“kama ukiangalia ile video kuna wimbo flani unalia kwa mbali mwanzo pale unaitwa ‘On My Way’ ndo wimbo niliokuwa naenda kushoot.” Alisema Joh Makini
Aliongeza kuwa mabadiliko hayo hayakumsumbua sana director ambaye alilazimika pia kubadili script na aliupenda zaidi wimbo wa ‘Nusu Nusu’. “Kitu kizuri ni kwamba hata nilipobadilisha wimbo bado director aliupenda tena wimbo niliomtumia, kwa hiyo kazi ikaendelea kuwa nyepesi tukabadilisha tu script, tukaandika script kufatana na wimbo husika tena”. Alimaliza
Home
»
Bongo star
» Wimbo unaosikika mwanzoni mwa video mpya ya Joh Makini ndio uliokuwa ufanyiwe video badala ya ‘Nusu Nusu’, ni collabo na msanii wa Nigeria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment