0
Kuna uvumi uliosambaa kuwa reality Tv show ya Big Brother Africa (BBA) ambayo huziunganisha nchi mbalimbali za Africa haitafanyika mwaka huu.
Meneja wa Multichoice Ghana, Anne Sackey amethibitisha uvumi huo na kusema kuwa ni kweli Multi Choice Ghana wamepokea ujumbe kutoka MNET kuwa shindano hilo halitafanyika mwaka huu.

Sackey ameongeza kuwa MNET hawakutoa sababu za kusitisha msimu mpya lakini yeye binafsi anahisi ni kutokana na ukosefu wa wadhamini.

Hata hivyo, watu wengi wanaamini kuwa hii inaweza kuwa ni ‘public stunt’ ya kuwaandaa watu na msimu mpya.

Source: Dailypost.ng

Post a Comment

 
Top