0
Mastaa wa Marekani wanaom-feel Wizkid wanazidi kuongezeka, baada ya Drake kuamua kufanya Remix ya hit song yake “Ojuelegba”, Alicia Keys na mumewe Swizz Beatz nao wamethibitisha kuwa ni mashabiki wa staa huyo wa Nigeria. Alicia Keys amepost video mbili Instagram akicheza nyimbo za Wizkid.



Katika video ya kwanza Keys amepost video ikionesha miguu yake na mumewe wakicheza ‘Carol’ na kuandika “Happy Feet jamming @wizkidayo”.



Na saa moja baaadaye alipost video ambayo inamuonesha akicheza kwa furaha wimbo wa Wizkid unaofanya vizuri sana kwa sasa “Ojuelegba” na kuandika, “This song makes me happy #goodvibes @wizkidayo”



Producer Swizz Beatz naye alipost cover ya Wizkid, “Ayo (Joy)” na kuandika “#vibes @wizkidayo”

Post a Comment

 
Top