0
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido amebadili mawazo ya kuachia album yake mpya dakika za mwisho.
Davido na Wizkid ni kama wanategeana kuachia album zao! Kwasababu kila mmoja amekua akisogeza tarehe mbele kila inapokaribia tarehe ambayo alitangaza.

Davido aliahidi kuwa album yake mpya ‘Baddest’ ingetoka mwezi wa 10 baada ya kuahirisha mara kadhaa, na Wizkid naye alipanga ingetoka September lakini baadae alisogeza hadi mwakani (2016) na kumuacha Davido aliyekuwa bado na mpango wa kuitoa mwaka huu.

Mwakilishi wa label yake ya HKN amesema kuwa Davido amelazimika kusogeza mbele kuachia album yake hadi mwakani kutokana na changamoto za ‘logistics’ wanazokumbana nazo kwenye label yake kwa sasa.

Post a Comment

 
Top