0
Diamond Platnumz ambaye amefanya collabo na msanii mkubwa wa R&B wa Marekani, Ne-Yo ameelezea hatua ilipofikia project hiyo inayotarajiwa kumfungulia njia ya mafanikio zaidi kimataifa.
Akizungumza na mtangazaji wa Citizen ya Kenya, Mzazi Willy Tuva, Platnumz amesema kuwa wimbo huo umekamilika lakini hawezi kusema utatoka lini kwa sasa kuna baadhi ya mambo ambayo anayoyaweka sawa kabla ya kuachia.

Diamond ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa tuzo ya MTV EMA ‘Best Worldwide Act Afrika/India’, amesema anafikiria kushoot video hiyo nchini Marekani pamoja na Africa.



Ne-Yo ambaye alikutana na kufanya kazi na Diamond wakati wa Coke Studio Africa jijini Nairobi, Kenya alikuwa miongoni mwa mastaa waliompongeza Baba Tiffah kwa ushindi wa MTV EMA kupitia Instagram kwa kuandika, “CONGRATS TO MY HOMMIE @diamondplatnumz for winning #BestWorldWideAct at the #MTVEMAs keep being great! Let’s go get em’ my guy!”

Post a Comment

 
Top