0
 
Baada ya Lebel ya msanii Diamond Platnumz WCB -Wasafi Records Kuwasainisha Harmonize na Raymond,Rapper Nay Wa Mitego amesema kuwa
panapo majaliwa miezi mitatu ijayo kwa kushirikiana na Free Nation na Team 966 Wataanza kuzunguka Mikoani kutafuta Wasanii Watatu Wakufanya kazi chini ya Lebel yake.

Nay amesema hayo kwenye Mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha “Extra Fleva” Ergon Elly wa Uplands Fm – Njombe mwishoni mwa wiki wakati wa tour yake ya SHIKA ADABU YAKO TOUR Mkoani Njombe.


Nay amesema kuwa uchache wa lebel za muziki Tanzania zinatokana na uchache wa wafanyabiashara wa muziki nchini wengi ni waimbaji wa muziki lakini safari ndio imeanza na baadae lebel zitakuwa nyingi tu.



Post a Comment

 
Top