0



Adam Juma Watanzania mnapenda vitu vizuri tu kulipa hamtaki, msiwaseme ma-director wadogo wapeni mahitaji yao acheni story.Katika utayarishaji wa video, Ili video ya muziki ikamilike kwa ubora unaotakiwa inahitajika bajeti nzuri ili director aweze kupata vifaa vizuri, location nzuri ambazo nyingi huwa ni za kulipia, kulingana na jinsi wimbo unavyohitaji na mambo mengine ya kiufundi zaidi.

Kwa ukweli huo maana yake ni kwamba hakuna video ambayo inaweza kufanyika bure, hata director akiamua kumsaidia msanii kwa kutomtoza pesa yoyote kama director, lakini atalazimika kulipia vitu vingine ili video ikamilike.

Director mkongwe Tanzania, Adam Juma wa Next Level amewatetea ma-director wadogo kuwa wanaweza kufanya vitu vikubwa endapo watapewa mahitaji yote yanayohitajika kuikamilisha video.


DOP jim bishop

Kupitia Instagram hiki ndicho alichoandika:

“My DOP jim bishop| watanzania mnapenda vitu vizuri vizuri tu kulilpa hamtaki, for years i have helped this industry na play role ya DOP n director, colorist, producer ili kazi iiende bila mapungufu! At that time wengine hata darasa la 7 hamjamaliza!!! Kama unataka quality badilikeni from directors to artist hakuna jinsi!! Msiwaseme madirector wadogo wapeni mahitaji yao acheni story. Nimewasupport wasani wengi sana for 10yr wengi mnajua! Km wewe nimsanii na unastatus give these new directors a chance to do big things!!!!!!! Give budget to get a DOP, a gud camera n post production!!! Sio jitu moja linafanya kila kitu alafu mnasifiana upuuzi tu hakuna anayekua!!!! Jim bishop amazing work buddie! Cost ya DOP tu ni $1500-$2000! I think mnapata picha kinainakuwaje!“

Video mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni zilizotayarishwa na AJ ni pamoja na video za Madee, Chegge na Temba ziliyofanyika Afrika Kusini, na video mpya ya Linex ‘Salima’ aliyomshirikisha Diamond ambayo imeshutiwa weekend iliyopita.

Post a Comment

 
Top