0
Baada ya kudondosha ‘Zigo’ wiki hii, Ambwene Yessaya a.k.a AY amesema mwaka huu atafanya kazi na wasanii wakubwa yaani A-list wa Marekani.
Tunapozungumzia wasanii wa A-list kwa Marekani tunawazungumzia watu kama kina Chris Brown, Kanye West, Nicki Minaj, Rihanna, Lil Wayne nk.

“Mwaka huu nataka nifanye kazi na A-List artists wa Marekani, nikisema A-List artists maana yake katika wale wasanii unaowajua wale wakubwa, sio B wala C,” alisema AY “Na kwaarifa yenu Sean Kingston sio A-list ni Blist, sasa nataka kwenda kwenye A-List artist”.

Kuhusu mapokezi ya wimbo wake mpya ‘Zigo’ uliotoka wiki hii, AY amesema umepokelewa vizuri sana hata nje ya Tanzania.

“Kikubwa kuhusu huu wimbo ni kuwa nilikuwa sijawahi kupata ile airtime ya radio katika nchi kama South Afrika, lakini jana nilikuwa naona tweets za watangazaji wanasema hawajui kiswahili lakini wameupenda huu wimbo, so nikaona kuwa okay hii kitu inaweza ikafika mbali zaidi ya pale ambapo inastahili kufika, na the way ambavyo mapokeo nimeyaona siku hizi unajua ni rahisi sana kujua wimbo wako umepokelewaje..nimeona katika mitandao ya kijamii watu wanavyo ijadili kazi.”


Zigo imetayarishwa na Nahreel na mixing kufanywa na Marco Chali. Watu wanasubiri kuona upande wa video ya wimbo huo utakuwaje.

Post a Comment

 
Top