0

Mapema mwishoni mwa juma lililopita Bobbi
Kristina ambaye ni mtoto wa marehemu
mwanamuziki wa Marekani Whitney Houston
alianguka bafuni na kukimbizwa hospitali huku
hali yake ikielezwa kuwa ni mbaya na kutakiwa
kukaa chumba cha uangalizi maalumu.
Imeelezwa kuwa hadi sasa hali yake bado ni
mbaya na madaktari wanaomuuguza katika
hospitali ya Emory University wamepoteza
matumaini na sasa wanaiachia familia yake
hatma ya maisha yake.
Bobbi Kristina akiwa na baba yake Bobby
Brown
Chanzo cha habari cha karibu kutoka ndani ya
familia hiyo kimedai kuwa hatma ya mtoto
huyo iko mikononi mwa baba yake ambaye
atatoa muamuzi kama atolewe mashine
zinazomsaidia kupumua au la licha ya
maamuzi hayo kuwa magumu kwake na kutaka
aachwe mwishoni mwa juma hili.
Baba wa mtoto huyo Bobby Brown ana imani
na kupona kwa mwanawe kwani katika familia
yao kuliwahi kuwa na mgonjwa ambaye alikua
na hali mbaya kwa muda wa siku nane lakini
alipona.

Post a Comment

 
Top