Muimbaji huyo amedai kuwa yupo jikoni kuandaa album itakayokuwa na nyimbo za jazz peke yake.
Mwasiti amedai kuwa atawashirikisha watayarishaji mbalimbali wa
muziki nchini kuandaa album hiyo . Miongoni mwa maproducer hao ni pamoja
na Nash Designer na Tudd Thomas.
Muziki wa Jazz si maarufu sana kwenye masikio ya Watanzania wengi na
ni miongoni mwa aina ya muziki mgumu zaidi kuufanya na huhitaji elimu
nzuri ya muziki kuweza kuumudu.
Muziki huo ulianzia kwenye jamii za Wamarekani weusi mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 21.
Wakati huo huo leo ni siku ya kuzaliwa ya Mwasiti.
No comments:
Post a Comment