Wawili hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata ujauzito wa Aunty iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe alikanusha.
Nakumbuka alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na Mose Iyobo, hizo taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio kama unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘
Pamoja na kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za instagram wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila……..?
Kingine kilichokolezea imani za wengi kwamba wawili hawa wapo mapenzini kweli ni Post ya Aunty Ezekiel siku ya Valentine ambapo alipost picha ya Mose na kuandika ‘Happy Valentine Moo akee Baby akee boo boo wa mm baba akee………. Jaden, Baba wa…………… Umbea tyuuuu nimemaliza waone kwanza, Aunty akee lv u‘
Aunty Ezekiel aliolewa zaidi ya miaka miwili iliyopita, unataka kujua anasemaje kuhusu ndoa yake wakati huu akiwa na ujauzito unaosemekana kuwa wa Mose Iyobo? bonyeza play hapa chini kumsikiliza
Post a Comment