Wema Sepetu na Ommy Dimpoz wanazidi kuumizwa vichwa watu.
Couples mpya ama ndio zile za project ziendelee? Yeah tunafahamu kuwa ushemeji hauna kikomo lakini hizi picha zinazoonekana ni kama zimevuka mpaka wa ushemeji. Maswali mengi kutoka kwa mashabiki wao ni kuwa ni kweli Ommy na Wema wameamua kuanzisha uhusiano licha ya ukweli kwamba Ommy ni rafiki wa karibu na Diamond Platnumz? Haijawahi kuwa kitu cha kawaida kwa rafiki kuwa na uhusiano na ex wa rafiki yake.
Hata hivyo Wema anaonekana kufurahia muungano huu kwakuwa ameshapost picha kadhaa akiwa hitmaker huyo wa ‘Tupogo’ kwenye akaunti yake ya Instagram zilizosababisha mrejesho wenye kishindo.
Jumatatu hii muigizaji huyo wa filamu amepost picha ya Ommy Dimpoz (hiyo juu) kama sehemu ya ‘Man Crush Monday’ (yaani siku maalum ambayo wanawake hutumia kuwataja wanaume wanaowazimia).
“So it’s a Monday already….. Y nat post my MCM….. Haiya Nalala now,” ameandika Wema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment