
Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora.
Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A’level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Vibe Tanzania inawaorodhesha baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…
Vanessa MdeeVanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.
Nisher Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.

Wema SepetuWema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.
Post a Comment