‘Nitazoea’ ni wimbo wa Mapenzi ambao umetayarishwa na ma-producer watatu ambao ni Aby Daddy, Lollipop na D-Classic.
Uongozi wa Mo Music umeiambia Bongo5 kuwa video ya ‘Nitazoea’ itaanza kufanywa wiki ijayo na Adam Juma wa Next Level.
Nyimbo za Mo Music zilizopita kabla ya huu ni ‘Basi Nenda’ ambayo ilifanya vizuri kila kona ya nchi, na kufuatiwa na ‘Simama’ pamoja na Almasi ambazo zilitoka kwa pamoja mwishoni mwa mwaka jana.
Post a Comment