0
Godzilla amewaonya vijana kuishi maisha yao wenyewe na sio kuiga ama kuumizwa na picha wanazoziona kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram.

Akiongea na kipindi cha Trending Africa cha Times FM, rapper huyo wa ‘Sala Sala’ alisema vijana wengi wanashawishika kuishi maisha yasiyo yao kwasababu ya kile wanachokiona kwenye mitandao hiyo.

“Social networks zinadanganya, sio kila kitu unachokiona ndio watu wanavyoishi,” alisema Zilla.

“Wengi wanadanganya na it’s a lie, amini moyo wako, believe in yourself, fanya maisha yako, anzisha lane yako watu wengine wafuatishe. Wasione demu eti demu kakaa na kapiga picha nzuri, wengine wanakaa kwenye nyumba za kupanga za rafiki zao maisha yao mabaya, it’s just a picture, isiharibu maisha yako. Mtu kapaki gari yake eti ‘Sea Cliff’ labda kaalikwa tu na washkaji haishi maisha hayo,” aliongeza.

“Kwahiyo watu wengi maisha yao wanayaharibu, vijana wengi wanafuatisha trend ya mastaa wanaishi vipi. Wengi wanaishi lakini wanaharibu mioyo yao, mioyo inavuja damu, wana huzuni.”

“Unaweza ukaona staa labda Bongo tuseme Diamond labda Wema Sepetu wanaishi poa lakini moyo wake una maumivu. Don’t believe in them, anzisha life yako in your own lane. Labda mtu kaona Jay Z na Beyonce wameshikana mikono, wanakumbatiana unaona hii ndio relationship goal yangu, lakini Beyonce na Jay Z wanapitia mambo mengi hapa kati wanaumizana wewe hujui, unaona tu picha wako pamoja.”

 sikiliza hapa

Post a Comment

 
Top