0
Wapo baadhi ya wasanii wa Tanzania ambao wameamua kuweka wazi mahusiano yao kwa kuwatambulisha wapenzi wao kwa mashabiki kwa kupost picha zao, au hata kuwataja kwenye Interviews pale wanapoulizwa kuhusu mahusiano, na kuna wengine ambao wameamua kuweka private mahusiano yao.
Muimbaji wa ‘Wanjera’ Ommy Dimpoz yuko kwenye orodha ya wasanii ambao hawajawahi kuyaweka wazi mahusiano yao.


Haijulikani kama huyu ndiye ‘wanjera’ wa ukweli au laa sababu Ommy alipost picha hii bila kuandika chochote.

Ommy Dimpoz amesema sababu za kwanini hajawahi kumtambulisha hadharani mpenzi wake.

“Sijapenda kuweka wazi sana swala la mahusiano kwasababu inatakiwa mimi niweze kuwa na uhakika kwamba huyu ambaye namtambulisha kwa wananchi ni kweli wakati umefika, kwasababu leo unaweza ukawatambulisha huyu baada ya siku tatu mambo hayaeleweki ukatambulisha mwingine, kwahiyo mwisho wa siku utaonekana kijana unatumia nafasi yako kuweza kuchezea watoto wa kike, kwahiyo najaribu kuwa makini kwa hilo lakini kipindi kitakapofika watu wataweza kufahamu kama Ommy ‘bae’ wake ni yupi” alimaliza

Post a Comment

 
Top