0
Muimbaji wa dancehall Patoranking kutoka Nigeria ambaye mwaka jana (2014) alikuwa miongoni mwa wasanii wa kimataifa waliotumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jijini Dar, ametajwa kuwa mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa Afrika wa mwaka kwenye tuzo za ‘2015 Vodaphone Ghana Music Awards’ (VGMA).
Tuzo hizo zimetolewa Jumamosi April 11, 2015 kwenye ukumbi wa Accra International Conference Centre (AICC) nchini Ghana.

Diamond Platnumz ndiye aliyekuwa akiiwakilisha Tanzania kwenye tuzo hizo katika kipengele cha ‘African Artiste of the Year’.

Wasanii wengine waliokuwa wakiwania kipengele hicho ni AKA (South Africa), Tiwa Savage (Nigeria), Yemi Alade (Nigeria) na Mavins (Nigeria).

Post a Comment

 
Top