0
Producer wa Tanzania aliyejipatia umaarufu nchini Kenya, Sappy amewaunga mkono wasanii wanaotafuta kufanya collabo za kimataifa kutokana na kile ambacho anasema ni kujijengea kujiamini katika muziki wao.
Sappy ambaye alianza kufanya kazi kwenye studio za Homeboyz Production kabla ya kuanzisha studio yake, Sappy Music Lab.

“Ni kitu kizuri sana na nimeangalia wasanii wengi waliofanya collabo na wasanii wa nje ya nchi imewasaidia sana katika muziki wao maana inawafanya wanapata njia tofauti pamoja na connection,” Sappy aliiambia E-News ya EATV hivi karibuni.

“Ukiangalia hasa wasanii wa Tanzania ambao wamefanya collabo na wasanii wa nje wamefanikiwa zaidi na pia wanakuwa wanapata mashabiki kutoka nchi nyingine kwahiyo ni kitu ambacho kinasaidia sana katika muziki.”

Post a Comment

 
Top