Rapper Shetta amedai kuwa alikuwa hategemei kama mashabiki wa muziki wangekubali uimbaji wake kwenye wimbo mpya ‘Shikorobo’ aliomshirikisha KCEE. Shetta alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV kuwa pamoja na msanii wa Nigeria KCEE kusifia uwezo wake wa kuimba, bado alikuwa na wasiwasi iwapo mashabiki wa Tanzania wangeupenda.
“Yaani mimi katika kitu ambacho sitegemei, kwanza sikutegemea kama watu watampokea Shetta akiimba,” alisema. “Sikutegemea kama watu watampokea Shetta akiimba.”
Video ya wimbo huo iliongozwa na Godfather na ilifanyika nchini Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment