“Ngoma zina utofauti ilipofika hii mimi ninashukuru kabisa ukisema kwamba imedrop nakubishia kwasababu, labda kama unasikiliza tu radio za Dar es salaam, kwasababu nasikiliza sana radio za mikoani, Interviews nyingi […] ukisema imedrop yaani hapo majibu yake sina kwasababu nina evidence nyingi za radio za mikoani, labda haija hit kama ‘Huko kwenu vipi’. Tofauti ya ngoma we sikiliza ‘Like Father Like Son’ na ‘Huko Kwenu vipi’ ni miziki miwili tofauti, miziki ya kubishanabishana mara nyingi inakuwaga inafika, Watanzania wanapenda vitu kama vile.” Stamina aliiambia Genge ya E-FM inayoongozwa na Ezden na Baghdad.
Aliongeza,
“Tumedrop hiyo (Like Father Like Son) kwaajili ya kuondoa ukimya pia, leo nimetoa ngoma hii, kesho nimetoa ngoma ya mapenzi, kesho kutwa nimeimba sijui siasa, muziki ndio unavyoenda sio tunaimba kitu kimoja kila siku hivyo hivyo.”
Post a Comment