“Kuna project nafanya kwahiyo ni album, kuna nyimbo ambazo nilizirekodi wakati bado sijajifungua na nyingine ndo nazimalizia nyimbo tatu za mwisho halafu ndo naanza kutoa, kwahiyo zimebaki nyimbo mbili. Itakuwa na nyimbo kumi na tano, kwahiyo kama nitazipunguza kidogo au kutoa zote sawa.” Alisema Besta a.k.a Mrs Marima.
Besta ambaye August 2013 alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kiume, amesema anazo sababu za kuamua kufanya album licha ya changamoto za soko la album za muziki Tanzania.
“Cha kwanza mi napenda kutoa album hata kama maslahi yamepungua kuna matatizo kwenye mambo ya album, lakini bado najua mashabiki wanahitaji kupata album, waone kazi sio kazi moja moja, na kwa upande wa kutoa hizo nyimbo nitaangalia kwasababu of course nafanya muziki na pia tunataka tutengeneze hela, kwahiyo ntatafuta njia nzuri ambayo itanifanya nitengeneze hela kupitia hizo nyimbo kwasababu kuna mambo mengi kuna ringtone kuna vitu vingi.”
Maproducer waliohusika kutengeneza album hiyo ni pamoja na Fundi Samweli pamoja na producer wa Uganda aliyekuwa akifanya nyimbo za Besta miaka ya nyuma.
“Studio nimefanya na sasa hivi kuna technology kwahiyo nimefanya na maproducer mbalimbali ambao wako nje, nimefanya pia na Fundi Saweli nyimbo nyingi na producer wangu wa Uganda.”
Kuhusu wasanii ambao amewashirikisha kwenye album hiyo amesema wapo lakini ni surprise.
Besta amesema kuwa mashabiki wajiandae kupokea wimbo wake wa kwanza miezi miwili kuanzia sasa, lakini video itachelewa kwa miezi mitano.
“Yaani haizidi miezi miwili wataanza kusikia wimbo ya kwanza, lakini video itachelewa kidogo kwasababu niko kwenye mazoezi, itakuwa baada ya miezi mitano hivi, lakini wimbo wa kwanza haitafika August utasikika.”
Post a Comment