0
Ni wasanii wengi wa Afrika wenye ndoto za kufanya kazi na wanamuziki wakubwa wa Marekani kama Trey Songz, lakini kwa Davido tayari ameamka na ndoto hiyo imetimia.
David Adeleke a.k.a Davido kutoka Nigeria amethibitisha kuwa tayari amefanya collabo na superstar mwenye idadi kubwa zaidi ya mashabiki wa kike, Trey Songz. Taarifa juu ya collabo hiyo ilianza kufahamika hivi karibuni baada ya orodha ya nyimbo za album yake mpya kuvuja kabla mwenye hajathibitisha.

Davido ameisifia collabo hiyo kwa kusema kuwa itapendwa zaidi na mabinti, ukizingatia Trey Songz ni msanii ambaye huwachanganya mashabiki wengi wa kike hata hapa Tanzania.

Davido alitweet: “ME AND @TreySongz RECORD LADIES GON LOVE THIS ONE!!!!”



Album mpya ya Davido ‘OBO’ inayotarajiwa kutoka mwezi ujao, itakuwa na collabo za wasanii mbalimbali wakubwa akiwemo Meek Mill, ambaye tayari wameshoot video ya wimbo huo.

Post a Comment

 
Top