Alipoulizwa kama Pacquiao aliponzwa na jereha kwenye bega lake la kulia, Mayweather anasema “Hakuna kitu kama hicho.” “Visingizio, visingizio, visingizio,” alisema.
“Alikuwa na kasi. Mkono wake kushoto ulikuwa kasi. Mkono wake wa kulia ulikuwa na kasi na alikuwa akiirusha yote kwa kasi na kwa nguvu.”
“I’m not going to buy into it, and I don’t want the public to buy into it.”
“Alipoteza,” Mayweather alisema. Anajua alipoteza. Nimeondoa heshima nyingi kwake baada ya hili.”
Mayweather anakiri kuwa awali alimtumia ujumbe mtangazaji wa ESPN, Stephen A. Smith kuwa anakubali mrudiano.
“Yeah, lakini nimebadilisha mawazo yangu,” alisema Mayweather. “Katika muda huu, hapana, sababu ni mkosaji aliyeumia na ni muoga. Kama ulipoteza, kubali kushindwa na useme ‘Mayweather, ulikuwa mpiganaji bora.’
Post a Comment