0
Rapper Kanye West (37) na mke wake Kim Kardashian (34) wanatarajia kupata mtoto wa pili.
Baada ya majaribio ya miezi kadhaa ya kushika ujauzito wa pili, Kim ameweka wazi kuwa ni mja mzito kupitia reality show ya Keeping Up With The Kardashians alipomueleza mdogo wake Khloe Kardashian juu ya majibu ya vipimo alivyofanya.

“I just got the blood test back and I am pregnant!” alisema Kim.

Kim na Kanye walipata mtoto wao wa kwanza wa kike North West June 15, 2013.

Post a Comment

 
Top