0

Producer na Msanii Baucha amesema amedhamiria kuanzisha mobile studio ili kuweka unafuu na urahisi wa ufanyaji kazi kwa wasanii wa Mikoani na Wilayani ambao walikuwa na ndoto ya kufnya wimbo/nyimbo kwenye studio kubwa Tanzania.

Katika Mahojiano aliyoyafanya weekend hii na Mtangazaji Ergon Elly wa Kitulo Fm – Njombe Baucha amesema kuwa wasanii wengi kutoka Mikoani wanatamani kuja Dar es Salaam kwaajili ya Kurekodi kazi zao lakini kutokana na Gharama za kuendesha maesha kwa kipindi chote cha kurekodi inakuwa kuwa wengi wemekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao katika muziki.


Baucha Records na timu nzimaya Baucha inatarajia kuanza kufanya kazi (Mobile Studio) katika mikoa mitatu ya kusini mwa Tanzania ambayo ni Njombe,Mbeya na Iringa na baadae mikoa mingine ya Tanzania.


Producers wengine ambao niliwahi wahoji kupitia HOT SHOW ya Highlands Fm Mbeya kuzungumzia mpango ambao unafanana na Baucha ni Man Water wa Combination Sound na Mr T wa Free Nation.

Post a Comment

 
Top