Lollipop aeleza kwanini haimbi muziki wa Bongo fleva licha ya kuwaandikia hits wasanii wengine
Mwandishi wa nyimbo pamoja na mtayarishaji wa muziki Lollipop ametoa sababu za kwanini yeye anaimba muziki wa gospel na si Bongo Fleva, licha ya kuwa ameshawaandikia hits wasanii wengine wanaofanya Bongo fleva.
Lollipop ndiye mwandishi wa ‘Siachani Nawe’ na ‘Nivumilie’ za Barakah Da Prince, pamoja na ‘Basi Nenda’ na nyingine za Mo Music.
“Muziki wa gospel kwangu mimi ni maisha kamili, lakini production pamoja na ishu za uandishi nimefanyika kuwa sehemu ya kazi yangu,” alisema Lollipop kupitia 255 ya XXL.
“As long as studio nakuwa nafanya kazi na watu tofauti, nafanya na wahindi wabudha, Mmasai akija na style yake ya muziki pia tutafanya kwasababu niko kazini, ile naichukulia kama kazi. Lakini kwa habari ya muziki wa injili ile ni maisha yangu kabisa, kwahiyo ukisikia nafanya gospel music sio kwamba nafanya kama kazi, kwangu ni maisha, ni kitu ambacho kinatoka ndani ya moyo wangu na ninapenda kufanya.” Alimaliza Lollipop.
Chanzo:-Bongo5
Post a Comment