0


Director Kevin Bosco Jnr aliyeongoza video mpya ya Mwana FA ‘Kiboko Yangu’
na zingine kibao, amemtabiria makubwa director mpya wa Bongo ambaye ameanza kuonesha dalili njema kupitia video chache alizofanya ikiwemo WCD ya kina Vanessa Mdee, pamoja na ‘Moyoni ‘ ya Navy Kenzo.

Director huyo wa Kenya aliulizwa ma-director wa Bongo anaowazimia:

“Kuna video flani na hata haijaongozwa na among AJ ama Nisher, I think ni maproducers wamekuja ma upcoming, wamefanya hii video ya ni latest hii imeshutiwa kijijini nilikua naona leo ya Navy Kenzo… Hanscanna.” Alisema Kevin kupitia 255 ya XXL.

“Hanscana he is the director to watch trust me, I know what I’m saying, he knows what he is doing. Kwasababu nimeangalia hiyo video niliyokwambia ndio kuna vitu flani zenye alipitisha lakini nampatia 90% kwa hiyo video, anajua kuchagua location, storyline inaenda hata mtu kama ni kiziwi anaweza akafuata ile stsory picha yake sio mbaya hachomi picha kama watu wengine I like what he is doing.”


Nickson George wa Clouds (kushoto) Director Hanscana (kulia)

Baadhi ya video ambazo amefanya Hanscana ni pamoja na Moyoni-Navy Kenzo, WCD-Vanessa Mdee+, Y-Tonny-Mama, G-Nako – Morale na zingine.


Post a Comment

 
Top