0
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/07/121.jpgNi mara chache sana kuona mtoto mwenye mwaka 1 na miezi mitatu kupiga kinanda ambacho
kinatoa fleva tofauti ambayo utadhani kimepigwa na mtu mzima.

Good news ninayotaka kukusogezea ni hii ya mtoto wa staa wa Bongo Fleva, H Baba anayeitwa Tanzanite amehusika katika kupiga kionjo kwenye single ya baba yake.

“Mimi nilichokifanya ni kwamba unajua mtoto unatakiwa umwangalie tangu akiwa mdogo na umtengenezea mazingira mazuri kwa hiyo nilichokifanya mimi nimemnunulia guitar, keyboard, game na meza yake nikamwekea pale kwa hiyo anachokifanya yeye ninakuwa namwangalie anafanya nini… kuna muda nilikuwa namwelekeza namna ya kupiga kinanda lakini siku hizi hataki mikono yangu, anapiga mwenyewe na guitar nilikuwa namwekea kwenye code hataki tena mikono yangu anapiga mwenyewe kwa hiyo mimi namwangalia tu, namrekodi clips zingine natupia Instagram.

Watu wanaona kwa sababu ni mtoto mdogo ana mwaka 1 tu na miezi mitatu kuna kitu ambacho anakifanya ni cha tofauti kwa hiyo lazima nimpe support kama mwanangu na pia nawashauri wasanii wenzangu wajifunze kupitia hilo wawape nafasi watoto wao… Usimfanye mtoto akawa haelewi baba yake anafanya kazi gani muweke mtoto aelewe Baba yake ni mwanamuziki naye atengeneze mazingira mazuri akiwa bado mdogo, audio imetengenezwa Fadha Get Music ambapo Tanzanite amepiga kinanda chake pale

Japokuwa producer kafanya kazi nzuri Mkolinto lakini Tanzanite kaonesha cha kwake kipo na nikiwa naenda kufanya interview nitakuwa nakiweka hicho kinanda kiwe kinasikika ili watu wajue amepiga kitu gani kwenye huo wimbo wangu unaoitwa ‘Show Time’ utakaotoka hivi karibuni’–-
alisema H Baba

Post a Comment

 
Top