0
Kila mtu huishi kwa kufuata ndoto yake nini inasema….Safari ya Muandaji wa Muziki kutoka
mkoani mwanza “Lollipop” wa K Records na Min Sound Studio amesema wakati ameanza kujihusisha na shughuli ya production alikuwa na ndoto za kuja kufanya kazi na msanii kutoka Kigoma na anayefanya poa na kazi yake ya “Mwana” Ali kiba hata ikiwa ni bure kutokana na uwezo wa msanii huyo.
Producer Lollipop amesema hayo wakati akifanya mahojiano katika kituo cha Redio Kitulo Fm Kilichopo Wilayani Makete Mkoani Njombe katika kipindi cha 97 Show kinacho endeshwa na Mtangazaji Ergon Elly.

Lolly ndiye mwandishi na Producer wa wimbo mpya wa Barakah Da Prince “Siachani nawe” akishirikiana na Kid Boy na Nusder na amewahi kuandika nyimbo za wasanii mbalimbali kama vile Mo Music n.k.…Ameongeza kuwa kila wimbo ambao anauandika na ku-produce unagharimu shilingi milioni Tano.

Post a Comment

 
Top