0
  
Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha
taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti la Mtanzania kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni kumtapeli shilingi milioni 10. Martin ameiambia Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.

“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin. “Kwa sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts, kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.

“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo story.”

Post a Comment

 
Top