0
Staa wetu TZ Jokate Mwegelo ambaye mwaka jana ni moja ya mastaa ambao milango ya neema ilifunguka upande wao kwa kusaini deal ya
kukuza biashara zake amesema mafanikio yalikuwa makubwa kutokana na mapokezi mazuri ya bidhaa zake sokoni.
 

Moja ya aina ya ndala ambazo zinauzwa na #Kidoti

Jokate alianza kwa kuuza nywele za kike na zenye brand name ya ‘Kidoti’, baadaye akaingia mkataba ambao umeongeza bidhaa nyingine sokoni TZ ikiwemo ndala ambazo zinapatikana kwa bei ambayo amesema haizidi shilingi elfu kumi.


                   Nikki Mbishi

Baada ya watu wengi kuongelea ishu ya Nikki Mbishi kutangaza kuacha muziki ameamua kurudi rasmi na kuachia ngoma yake mpya ambayo itatoka wiki ijayo na baada ya hapo kutakuwa na tour yake ya kimuziki kwenye maeneo mbalimbali TZ.


Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake, Shilole.

Nuh Mziwanda ameomba radhi kutokana na picha ambayo aliiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, watu wakatoa comment ambazo anahisi kwamba walielewa vibaya picha hiyo, Nuh amesema sababu ya kuweka picha hiyo ilikuwa kama kuwatangazia fans wake kwamba kuna video ya wimbo mpya inakuja na picha hiyo ilikuwa ni sehemu ya behind the scene ya video hiyo.

Post a Comment

 
Top