0
King Maluu, mwanamuziki aliyepiga kibwagizo kwa kutumia kifaa cha Saxaphone kwenye ngoma ya Ommy Dimpoz ‘Tupogo’ amesema wimbo huo ulimpa mashavu mengi.

Akizungumza na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, King Maluu amesema katika utengenezaji wa wimbo huo alilia kutokana na jinsi wimbo ulivyo na hisia.

“Mpaka na mwili unanisisimka ndio umenipatia jina kubwa sana,” alisema Maluu. “Bado ndio imenitambulisha kote kote. East Africa, Tupogo ni wimbo niliopiga halafu nilipiga nikalia kwenye studio. Niliga ile melody ikanigusa mpaka machozi yalinitoka, sijui ni kwanini kwa sababu ilitokea pale sijui wanasema ni vuvuzela na kumbe sio ni vuvuzela hii ni Saxaphone. Sasa kile kitu kilinigu sana sana watoto wananiambia napiga mimi vuvuzela nikapiga kwa feeling kali sana na hata kama ukisikia mlio wake ni mkali mno.”

Post a Comment

 
Top