0
Mwimbaji nyota wa Jahazi Modern Taarab Fatma Mohamoud maarufu kama Fatma Mcharuko au Fatma Nyoro, Alhamisi iliyopita alikwaa jukwaa la Mashauzi Classic ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.
 


Katika kile kinachoonyesha wazi kuwa makundi hayo mawili ya taarab yenye mashabiki wengi zaidi hayana bifu, mkurugenzi wa Mashauzi Classic akampandisha jukwaani Fatma Mcharuko ili kuwasabahi mashabiki na kuwapa ladha kidogo ya ngoma za Jahazi.

Fatma Mcharuko akaimba kipande cha wimbo wake “Aso Kasoro” ambao ulipagawisha ukumbi mzima.

Lakini mashabiki wakapagawa zaidi pale mwimbaji huyo alipokumbusha juu ya onyesho la Jahazi na Mashauzi Classic litakalofanyika Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu kwenye ukumbi wa Travertine ambapo akasema si mpambano ila kufunikana imo …mashabiki wakalipuka kwa furaha.



Baadhi ya watu wengine wa Jahazi waliokuwepo ndani ya ukumbi wa Mango Garden ni mkurugenzi msaidizi Hamis Boha na mpiga solo Emeraa ambaye nae pia alipanda jukwaani kupiga wimbo wa “Aso Kasoro”.

Isha akimtambulisha Fatma Mcharuko

Fatma Mcharuko akichekwa kwa maneno ya Isha

Fatma Mcharuko akiongea machache

Emeraa Solo wa Jahazi akimpigia gitaa Fatma Mcharuko

Mcharuko akipandisha watu mzuka

Mashabiki wakipagawa na uimbaji wa Mcharuko

Fatma Mcharuko akimkumbatia Isha kwa furaha mara baada ya kumaliza kuimba

Hapa akipozi na Zubeida Malick

Mkurugenzi msaidizi wa Jahazi Hamis Boha akipozi na Isha Mashauzi

Hapa Fatma Mcharuko anacheza goma la Mashauzi

Post a Comment

 
Top