0
Muimbaji wa kike Mcongo Alicios Theluji ambaye ni hit maker wa ‘Mpita Njia’ ft. Juliana Kanyomozi na ‘Posa ya Bolingo’, ni miongoni mwa wasanii waliotoa burudani kwenye show ya Christian Bella iliyofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam weekend iliyopita.

Alicios akitumbuiza kwenye kwenye show ya Christian Bella Ujio wa Alicios nchini umempa msanii Barnaba fursa ya kukutana naye na kuweka mipango ya kufanya collabo.

Barnaba ameiambia Bongo5 kuwa amefanya mazungumzo na Alicios ambaye tayari ameondoka nchini, na wamekubaliana kuwa Barnaba afanye sehemu yake na amtumie ili aweze kuingiza sauti yake kwenye wimbo huo.


Alicios na Diva The Bawse

Kupitia Instagram Barnaba amemshukuru Diva Tha Bawse kwa kumuunganisha na msanii huyo.

“Special Thanks to My Mom @divathebawse lol this is My first long distance collaboration . one of the most powerful and beautiful song coming feat @alicios isingewezekana bila wewe mama yangu @divathebawse Bless You Momi @bongofive @Bongo5″.

Alicios ni Mcongo lakini anaishi nchini Kenya toka akiwa mdogo.

Post a Comment

 
Top