0
Mwishoni mwa mwaka uliopita kulikuwepo na tetesi kuwa Beyoncé na Jay Z walikuwa studio kurekodi album yao ya pamoja.
Huenda mwaka huu album hiyo ikaingia sokoni.

Kwa mujibu wa DJ Skee, album hiyo ipo mbioni kukamilika na itatolewa kupitia mtandao wa TIDAL unaomilikiwa na Jay Z.

Tayari miradi kadhaa ya Jay Z na Beyonce imeshawekwa kupitia TIDAL peke yake ikiwemo video ya Glory na wimbo Die With You.

Post a Comment

 
Top