0
Rapper wa Weusi, Joh Makini Ijumaa iliyopita (April 24) video ya wimbo wake mpya ‘Nusu Nusu’ iliyofanywa Afrika Kusini ilitambulishwa ‘exclusively’ kwenye kituo cha kimataifa MTV Base na mapokeo yake yamekuwa ni mazuri kutoka kwa mashabiki mbalimbali ambao wamesifia wimbo na video.
Joh amezungumza kuhusu video hiyo iliyoongozwa na director aitwaye Justin Campos ambaye pia ndiye aliyeongoza video ya Vanessa Mdee ft. K.O ‘No Body But Me’ pamoja na ‘Taking Over Me’ ya staa wa Nigeria Yemi Alade .

“Matarajio yamekuwa ni makubwa sana kuliko hata vile nilikuwa nimedhani mwanzo, kwasababu unajua unaposhoot video ni jambo la kwanza lakini jambo la pili ni kama hiyo video inaweza ikashootiwa katika kiwango ambacho ulihitaji, manake wakati mwingine pia unaweza ukaweka hela video ikashootiwa lakini isiwe kali. “ Alisema Joh Makini.

Hit maker wa ‘XO’ amesema kuwa katika video zake zote alizowahi kufanya, video ya ‘Nusu Nusu’ ndio anaipa nafasi ya kwanza kwa ubora.

“Kwahiyo video ilipokuja kusema ukweli mimi mwenyewe niliiangalia nikaipenda, to be honest nadhani katika video zangu zote ambazo nimefanya kwenye muziki nafikiri hii naipa namba moja katika ubora wa video ambazo nimewahi kufanya mpaka sasa hivi. Na mapokezi yake yamekuwa ni makubwa ukichukulia imepokelewa nje na ndani ya nchi kwa wakati mmoja, tofauti na video zingine ambazo nimekuwa nikizifanya. Kwangu naichukulia kama hatua naichukulia pia ni hatua kubwa pia katika muziki wa hip hop wa Tanzania kwenda kwenye level za kimataifa sasa hivi.”

Ameongeza kuwa baada ya MTV Base, wiki hii inaweza kuanza kuoneshwa kwenye vituo vingine vya kimataifa ikiwemo Trace TV ya Ufaransa pamoja na SoundCity ya Nigeria.

Joh pia amewashukuru watu mbalimbali waliomsupport hadi kufanikisha video hiyo wakiwemo wasanii wenzake alioenda nao Afrika Kusini.

“Ningependa niwashukuru timu nzima ambayo tulisafiri kwenda South Africa, Vanessa, G-Nako, Jux, Nareel, Aika na Shetta pia ambaye alikuja siku ambayo tulikuwa tunafanya video, kwasababu kwa kuwepo kwao pale na tukichangia mawazo na tukifanya kazi kama timu ndo maana tulipata kitu bora kila mtu alikuwa ana moyo wa kujituma ili kuhakikisha hii video inakuwa katika kiwango kinachotakiwa. Lakini pia kwa mashabiki wangu kwasababu support yao wamekuwa wakisupport muziki wa Joh Makini ndio imenipa nguvu ya mimi kusafiri na kwenda kufanya hii video kubwa kwaajili ya wao kuona kwamba na Joh Makini sasa anakuwa anaupeleka muziki wa Hip Hop kwenye level tofauti na waliyozoea.”

Post a Comment

 
Top