0
Mfanya biashara na rapper Shawn Corey Carter maarufu kwa jina la Jay Z ameibuka kuutetea mtandao wake wa kusikiliza nyimbo ‘Tidal’ uliozinduliwa mwezi uliopita, baada ya ripoti kudai kuwa haufanyi vizuri (ume-flop).
Ripoti hizo zilidai kuwa ku-flop kwa Tidal ni hujuma iliyofanywa na wapinzani wake kama Spotify na Apple baada ya kuona kama imekuja kuwaharibia biashara.

Jay Z ametumia akaunti yake ya Twitter yenye followers zaidi ya milioni 3 kuwaondoa hofu huku akitumia hashtag ya #TidalFacts.

Kwenye moja ya tweet hizo aliandika kuwa Tidal iko vizuri na imefikisha subscribers zaidi ya 770,000 ikiwa hata mwezi haujaisha toka wazindue biashara hiyo.

“Tidal is doing just fine. We have over 770,000 subs. We have been in business less than one month. #TidalFacts”.

Katika tweet nyingine Jigga aliwaomba watu waipe nafasi Tidal ya kukua huku akitolea mfano kuwa hata iTunes haikujengwa siku moja, na Spotify imechukua miaka 9 kupata mafanikio, hivyo kuwaomba watu waipe nafasi Tidal ikue.

Hii ndio mvua ya Tweet za Jay Z zenye maelezo ya kuitete Tidal.




Post a Comment

 
Top