0
Rapper mkongwe Nas ametangaza kuachia album mpya mwaka huu (2015) ikiwa ni miaka mitatu imepita toka alipotoa album yake ya sita.
Nas ametoa habari hiyo akiwa kwenye show huko Orlando, Florida, Marekani weekend iliyopita.

“Right muthaf**kin’ now, death to all snitches. Watch every n***a around you my n***as ’cause s**t is real out here. 2015, new album this summer,” alisema Nas.

Mwakilishi wa label yake ya Mass Appeal Records amethibitisha kuwa album hiyo itatoka kupitia Def Jam.

Album ya mwisho ya kutoka kwa Nas iitwayo ‘Life Is Good’ ilitoka mwaka 2012 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200, na iliuza nakala milioni 14.3 Marekani.

Post a Comment

 
Top