0
Hillary Clinton ameshatangaza nia ya kugombea urais mwaka 2016 lakini huenda akakutana na upinzani kutoka kwa Mmarekani mweusi mwingine kama ilivyokuwa kwa Barack Obama mwaka 2008!
Hata hivyo huyu si mshindani unayeweza kumdhania  ni rapper!

November mwaka 2012, Waka Flocka Flame alitweet: I’m dead ass running for president in 2016.” Na sasa amethibitisha kuwa hakuwa anatania.

Jumatatu hii, rapper huyo amezungumza na Rolling Stone kuelezea nia yake ya kuwa mgombea wa urais wa Marekani mwakani. Mgombea wake mwenza amemtaja kuwa ni DJ Whoo Kid.

Akiwa rais, Waka amesema jambo la kwanza atakalofanya ni kuhalalisha bangi!

Post a Comment

 
Top